Stories of imaginary kingdoms in Shaaban Robert looks at the society,
explores systems of governance and responsibilities of rulers and the
citizens. Kwa zaidi ya miaka kumi na tano vitabu vya mwandishi maarufu
kushinda wote katika jamii za Waswahili kote Afrika ya Mashariki na
Kati, Marehemu Sheikh Shaaban Robert, havikupatikana Tanzania. Sababu
ya kukosekana kwa vitabu hivyo ni kuwa kampuni ya kigeni
iliyovichapisha iliamua kuacha kuvichapisha kwa sababu haikulipwa kwa
fedha za kigeni jambo, lililosabishwa na hali mbaya ya uchumi. Athari
za kupotea kwa vitabu vya Sheikh Shaaban Robert katika miaka hiyo ni
kwamba Watanzania wengi hasa wale wenye umri chini ya miaka
thelathini, hawamjui mwandishi huyu maarufu na hawakulelewa katika
mazingira ya utajiri wa maandishi yake ambayo bila shaka yoyote ni
mfano pekee wa utajiri wa urithi wa utamaduni wetu. Kwa kuvichapisha
vitabu vya Marehemeu Sheikh Shaaban Robert tunawakaribisha tena
Watanzania, hasa vijana kuvisoma, kuburudishwa na kufunzwa na yale
aliyoyaandika kwa sanaa na kipaji adimu.
Les mer
Produktdetaljer
ISBN
9789987449149
Publisert
2023
Utgave
1. utgave
Utgiver
Vendor
Mkuki na Nyota Publishers
Språk
Product language
Annet
Format
Product format
Digital bok
Forfatter